Mkuu wa Wilaya Musoma Dkt. Alfan Haule Leo Septemba 26, 2023 katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Musoma ametoa tahadhari ya
uwepo wa ugonjwa wa Kutapika na Kuharisha katika Halmashauri jirani ya Rorya na hivyo kutaka kuweka mikakati ya kuondokana na janga hili kabla halijafika katika Halmashauri yetu. "Ni Bora tutumie nguvu nyingi katika kujiepusha na gonjwa hili kuliko kulitibu." Amesisitiza Dkt. Haule pamoja na kuwataka watendaji katika ngazi ya Halmashauri pamoja na vijiji kutoa Elimu Kwa wananchi juu ya ugonjwa huu.
Amesisitiza hatua madhubuti za kudhibiti ugonjwa huu zichukuliwe mapema ikiwa ni pamoja na uwekaji wa ndoo za maji na sabuni kwenye taasisi zetu Kwa ajili ya usafi wa mikono ikiambatana na sehemu za kutolea huduma za chakula Kwa Wananchi( Hotelini, magenge, minadani pamoja na sehemu zenye mikusanyiko ya watu).
"Ni lazima tufanye oparesheni ya usafi na kuhakikisha Kila kaya ina choo na kukitumia". Amesisitiza Dkt. Haule na kuwataka watendaji wa Serikali kuchukua tahadhali zote Ili kuzuia gonjwa Hilo ambalo ni tishio kwa Wananchi.
Musoma Town opposite to Airport
Sanduku la Posta: P.o. Box 344 Musoma
Simu: 0282622163
simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@musomadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Haki zote zimehifadhiwa